Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, April 3, 2015


 Snoop Dogg Picture Leads To Punishment For Texas Trooper
Picha aliyoiweka katika Instagram rappa toka pande za Long Beach, California  Snoop Dogg imemponza afisa usalama wa Texas.Afisa huyo wa usalama anayetambulika kwa jina la Billy Spears,aliweka pozi na kupiga picha na rappa Snoop Dogg na baadaye rappa huyo akaiweka katika akaunti yake ya Instagram kitendo kilichopelekea kumuweka afisa huyo katika wakati mgumu baada ya wakuu wa idara yake kuiona picha hiyo na kumpatia adhabu.
 Taarifa zaidi zinasema,sababu kubwa za afisa kupewa adhabu ni kuweka pozi na kupiga picha na mtu maarufu ambaye rekodi yake ni mbaya haswa katika maswala ya dawa za kulevya na amekuwa akijitangaza kuwa ni mpenzi wa kutumia kiasi kikubwa cha bange.

katika utetezi wake afisa huyo wa usalama bw Billy Spears amesema,alikubali alipoombwa kupiga picha ila hakujua mtu huyo ni nani.

Snoop Dogg na afisa huyo wa usalama walipiga picha hiyo huko Austin,Texaskatika tamasha la muziki la South By Southwest music festival in Austin.
Tazama picha hiyo hapo chini:
 Snoop Dogg Texas Trooper


0 comments:

Post a Comment