Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, May 4, 2015

 Image result for jay z,eminem & drake
Mtandao unaojihusisha na maswala ya muziki,Billboard,umeandika orodha ya wanamuziki ambao wameingiza pesa zaidi kupitia muziki na upande wa muziki wa Hip Hop kwa mwaka 2014.

Rappa Jay Z ametajwa kushika nafasi ya 9 huku makusanyo yake kwa mwaka 2014 yakitajwa kuwa ni  dolla millioni 22 ambazo ameingiza dola 1.2 kwa mauzo ya muziki na zaidi ya dola millioni 19 kwa ziara za muziki.
Anayefuata katika orodha hiyo ni Eminem ambaye ameshika nafasi ya 20 kwa kuingiza kiasi cha dolla millioni 11.9 akifuatiwa na rappa Drake ambaye ameshika nafasi ya 21 kwa kujiingizia kiasi cha dolla millioni 10.6 ambazo alizipata kupitia kuuza kazi zake na kufanya ziara za muziki zikiwemo "Would You Like a Tour?" na "Drake Vs. Lil Wayne" .
Beyonce ambaye ni mke wa Jay Z ameshika nafasi ya 12 kwa kujiingizia kiasi cha dolla millioni 19.6 ambapio inaonekana Beyonce anaingiza mkwanja zaidi ya mumewe katika vipengele vingi ukiachilia ziaraza muziki.


Rihanna ametokea katika orodha hii na kushika nafasi ya 32 tofauti na mwaka uliopita ambapo alikuwa katika nafasi ya 20.





0 comments:

Post a Comment