Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, May 6, 2015

 Image result for Puff Daddy & Dr. Dre
Gazeti la habari za biashara la nchini America,Forbes,limeweka orodha ya wana Hiphop 5 matajiri zaidi kwa mwaka 2015 ambayo imetawaliwa na majina yaliyotamba mwaka jana.
Forbes imetaja wana Hiphop watano matajiri zaidi ambao ukiachilia mbali muziki ni wafanya biashara ambao wanamiliki makampuni ama viwanda.

Puff Daddy ambaye anatajwa kuongoza orodha hiyo kwa miaka 5 sasa,anamiliki vyombo vya habari vya Revolt,Televisheni na mtandfao,pia anadili na wauzaji wa vinywaji vya Diageo,Ciroc na hivi karibuni amezindua the fitness water Aquahydrate.Utajiri wa Diddy ni zaidi ya dola millioni 725.
Dr. Dre ameshika nafasi ya pili katika orodha ya wanaHiphop matajiri zaidi mwaka 2015, ukiweka mbali shughuli za muziki,Dr Dre amelipwa takriban dolla millioni 700 kama malipo ya mauzo ya Beats.


Jay Z ameshika nafasi ya tatu mwaka huu kwa kuwa na kiasi cha dolla millioni 550 alichojiingizia kutokana na shughuli zake za muziki,ziara na matamasha na kama haitoshi wasanii wake wa Roc Nation.
50 Cent ameshika nafasi ya nne kwa kuwa na mkwanja kama dolla millioni 155 million alizojiingizia kupitia dili lake na nguo za ndani za Frigo, Effen Vodka na vifaa vya kielektroniki vya SMS audio.
Cash Money Records CEO Birdman' mwenye dolla millioni150 anakamilisha orodha ya "Forbes Five" 


Tazama orodha ya wanaHiphop 5 matajiri zaidi2015:
1. Diddy - net worth: $725M
2. Dr. Dre - net worth: $700M
3. Jay Z - net worth: $550M
4. 50 Cent - net worth: $155M
5. Birdman - net worth: $150M

0 comments:

Post a Comment