Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, March 30, 2016

 Tokeo la picha la 50 cent rick ross
Kinachoendelea kuwahusu masta 50 Cent na Rick Ross nikesi ya madai ambapo rapa 50 Cent amemtaka Rick Ros kumlipa kiasi cha dola millioni 2 kwa kosa la kutumia biti ya hit yake, "In Da Club" katika mixtape aliyoipa jina Renzel Remixes.
Ross alihudhuria mahakani juzi (March 28) na kumuomba hakimu atupilie mbali kesi hiyokwa kusema kwamba anaamini kesi hiyo ni kama kisasi kutokana na 50 Cent kufunguliwa mashataka ya kesi ya madai kwa kile kilichosemekana kumdhalilisha baby mama wa Rick Ross,bi Lastonia Leviston,ambaye alishinda kesi hiyo iliyopelekea rapa 50 Cent kutakiwa kumlipa mama huyo fidia ya dola millioni 5 na dola millioni 2 kama adhabu.
Akiendelea kujitetea bosi huyo wa The Maybach Music Group alisema kwamba alitoa mixtape hiyo ya  Renzel Remixes for free hivyo hakutengeneza mkwanja wowote kupitia project hiyohuku akiongezea kusema 50 hana haki ya kumdai malipo ya kutumia biti hiyo ya "In Da Club".
Upande wa 50 Cent ulifungua kesi ya madai ukidai  Ross alitumia biti ya In Da Club katika mixtape hiyo ili  kuipromote albamu yakeya  Black Market.albamu ambayo ilishika namba 6 katika  Billboard's Top 200 albums chart, kwa kuuza nakala zaidi ya 64,000ndani ya wiki.

0 comments:

Post a Comment