Jambo mambo hayakuwa mazuri pale walimpotaja rappa Kendrik Lamar kuwa rapa bora wa mwaka, jarida la GQ limemtaja Pharrell Williams kuwa ndiyo Hitmaker Of The Year kwa mwaka 2013.
Zoezi la kumpitisha Pharrell Williams kuwa ndiyo Hitmaker Of The Year halikuwa gumu kwani poducer huyo ametengeneza hits za kutosha zinazosumbua kuanzi vituo vya radio mpaka ma club.
Mapema mwaka huu Pharrell alimtengenezea Robin Thicke wimbo gumzo wa "Blurred Lines," wimbo ambao umevunja records mbalimbali kwa mauzo kwani ndani ya wiki ilinunuliwa na kusikilizwa na watu wasiopungua millioni 228.9.Superproducerpia akatengeza wimbo wa Daft Punk "Get Lucky." ambayo nayo ilipata sifa ya mauzo ya multi-platinum.
Williams pia amehusika na utengenezaji wa albamu ya Jay Z,Magna Carta Holy Grail ambayo pia mauzo yake yalifikia platinum siku ya kwanza ya kuachiwa.
Wednesday, November 20, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment