Curtis Jackson aka 50 Cent ambaye ni rapa,muigizaji wa filamu na mjasiliamali akiwa bado hajatoa albamu yake ya sita na inayosubiriwa muda mrefu ya Street King Immortal,amesema anajikita zaidi katika sanaa ya uigizaji na uzalishaji wa vipindi.
akiongea na waandishi wa Muscle & Fitness magazine aliwaelezea ni namna gani ameweza kuendelea kuwa mkakamavu kiafya lakini pia aliongelea mipango yake katika muziki na filamu kwa kusema :nataka kumalizia albamu yangu ya sita [Street King Immortal] na sina mpango wa kuweka rekodi nyingine kama wasanii wengine wanavyowish sababu nshauza mamilioni ya nakala.
50 pia alizungumzia kinachoendelea katika tamthilia ya Hiphop inayoonyeshwa katika televisheni ya FOX, Empire jinsi inavyoshindanishwa na tamthiria yake ya Power na kusema: “Empire wamegeza kilakitu kutoka Power kuanzia idea ya story mpaka marketing tu kwasababu wametaka kuwapata watazamaji wa Power,amesema hana tatizo na waigizaji ( cast) ila haoni kama Empire inajiendesha.
50 alitishia kuacha kutengeza tamthria za Power mapema mwezi huu baada ya kutotajwa kuwania tuzo za Golden Globe nominations.
50 katika kuthibitisha anaelekea kustaafu rap na kujikita zaidi katika filamu na uzalishaji wa vipindi vya filamu amesema yupo katika maongezi ya kushiriki katika filamu Predator na kusema washaongea na director Shane Black’.
0 comments:
Post a Comment