Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, April 30, 2014

 
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini sheria hio licha ya malalamiko kutoka kwa vikundi vya wanawake nchini humo.Taarifa kutoka katika ofisi ya Rais ilisema kuwa mswada huo ambao unaojumuisha vipengee kadhaa kuhusu ndoa , imekuwa sheria sasa.
Mswada huo ulioleta mageuzi katika sheria ya sasa , ilipitishwa na bunge mwezi jana kuidhinisha rasmi utamaduni wa ndoa ya zaidi ya mwanamke mmoja.
Wakati mswada huo ulipopitishwa mwezi jana , wabunge wanawake waliondoka bungeni kwa Hasira baada ya mjadala mkali.
Viongozi wa baadhi ya makanisa pia wamepinga vikali mswada huo.
Shirikisho la kitaifa la mawakili wanawake pia limesema kuwa litapinga sheria hiyo mahakamani.
Katika sehemu nyingi barani Afrika, kuoa zaidi ya mwanamke mmoja ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi sawa na hali ilivyo nchini Kenya

0 comments:

Post a Comment