Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, January 16, 2015

Aaliyah-gallery-12

Aaliyah angekuwa anatimiza miaka 36 leo Jan. 16.

Aaliyah alitunukiwa u Princess wa R&B akiwa na umri wa miaka 22 tu na alishaingia katika kuwania tuzo kubwa duniani za Grammy.Muimbaji huyu alifariki  August 25, 2001,huko Marsh Harbour, Bahamas katika ajali mbaya ya ndege.


Sade-Best of Sade.jpg
Helen Folasade Adu (amezaliwa 16 Januari 1959) ni mwanamuziki kutoka nchi ya Nigeria. Anajulikana zaidi kwa jina la Sade. Sade ambaye amewahi kupata Tuzo ya Grammy hasa ni mwimbaji na mtunzi.
Sade alizaliwa katika mji wa Ibadan katika Jimbo la Oyo. Baba yake, Bisi Adu, alikuwa ni Mnigeria, mhadhiri wa masuala ya uchumi, na mama yake, Anne Hayes, alikuwa ni nesi toka Uingereza. Baada ya baba na mama yake kuachana, mama yake alirudi Uingereza ambapo aliwachukua Sade na kaka yake, Banji. Akiwa Uingereza, Sade alijenga mapenzi na masuala ya mitindo, dansi, na kuimba. Wakati huo alipenda kuwasikiliza wanamuziki kama Marvin GayeCurtis Mayfield, na Donny Hathaway.

0 comments:

Post a Comment