Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, April 24, 2014


  

 Jarida la People huchapishwa kila wiki nchini Marekani na kusomwa na watu wanaokaribia milioni 40
Jarida hilo limemtaja Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014.
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu '12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki hii ya jarida hilo.
Katika orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku waigizaji maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika filamu hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5 mtawalia.Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Tuzo hii ya kivyake kwa muigizaji huyo imegonga vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufikia chochote maishani mwao.

0 comments:

Post a Comment