Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Saturday, May 3, 2014

 
Mtandao wa BBC.com inaripoti Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya Jumapili akiwa uwanjani.
Dani ni raia wa Brazil anayesakatia soka yake katika klabu ya Barcelona.
Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati Alves alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili.
Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii.
Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.
Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.

0 comments:

Post a Comment