Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Tuesday, January 27, 2015

Lil Wayne, Drake, and Nicki Minaj
Lil Wayne amekuwa katika harakati za kutaka kujitoa katika lebo inayommiliki ya Cash Money.
Bosi huyo wa The Young Money,Lil Wayne pia ametangaza kumshitaki bosi wa Cash Money,Birdman kwa kile anachokiita kumzuia kama mateka,kumcheleweshea kazi zake hasa albamu ya Tha Carter V na  pia anamdai kiasi kisichopungua dolla millioni 8.
Sambamba na mashitaka hayo,Lil Wayne pia atafungua mashitaka zidi ya Birdman kuhusu uhalali wake wa kuwamiliki wasanii walipo katika lebo yake ya Young Money ambao ni Drake,Nicki, Christina Milian, Lil Twist na Mack Maine.
Weezy anaamini ikiwa ataondoka Cash Money ataondoka na wasanii hao kwasababu mkataba alisaini nao yeye kama bosi wa Young Money.
Kufuatia kucheleweshwa kwa albamu ya Tha Carter V,Lil Wayne ameachia mixtape inayokwenda kwa jina la Sorry 4 the Wait 2.

0 comments:

Post a Comment