Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, January 22, 2015

Usiku wa kihistoria katika muziki unazidi kunogeshwa. Usher, Pharrell Williams, Common, John Legend, na Sam Smith wameongezwa katika orodha ya wanamuziki watakaotumbuiza katika sherehe za 57 za utoaji wa tuzo zaGrammy.
Mshindi mara 8 wa tuzo hizo za Grammy na aliyetajwa kuwania tuzo hiyo mara nne katika tuzo za mwaka huu,Usher atashambulia jukwaa  huku mtajwa kwa mara ya kwanza katika tuzo hizo aliyetajwa kuwania tuzo mara 6 mwaka huu,muimbaji wa uingereza,Sam Smith,naye atatumbuiza.
Sambamba na Usher na Sam Smith,Pharrell,ambaye pia ametajwa kuwania tuzo hizo mara sita naye atatumbuiza. 
Common na John Legend wataungana jukwaani kutumbuiza wimbo wao “Glory”,mbali na kutumbuiza,Common ametajwa kuwania tuzo za Best Rap/Song Collaboration kwa wimbo “Blak Majik” na Best Rap Album kwa albamu Nobody’s Smiling.
Wengine watakaotumbuiza katika sherehe za 57 za utoaji wa tuzo hizo kubwa kabisa duniani za Grammy zitakazoongozwa na rappa LL Cool J ni sambamba na Madonna, Ariana Grande, Ed Sheeran, Miranda Lambert, AC/DC na Eric Church.
Tamasha la utoaji wa tuzo za Grammy mwka huu zitafanyika siku ya jumapili tarehe 8 mwezi Febkatika ukumbi wa Staples Center huko Los Angeles.

0 comments:

Post a Comment