Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Tuesday, February 10, 2015

Family to let Bobbi Kristina die on same day as Whitney

Ndugu na wanafamilia wa mtoto pekee wa mastaa waimbaji,Whitney Houston na Bobby Brown,Bobbi Kristina Brown 21,wamekubaliana kuwaruhusu madaktari na wauguzi wa hospitali alipolazwa binti huyo,kumuondolea mashine maalumu za kumsaidia kupumua kwani tangu awekewe mashine hizo hajaonyesha dalili za kupata nafuu.
Bibi wa Bobbi,Cissy Houston ndiye aliyetoa wazo la kuruhusu mashine hizo kutolea siku ya tarehe 11 Feb tarehe sawa na siku aliyofariki mama yake,Whitney Houston mwaka 2012.
Wanafamilia wamesema kwa kufanya hivyo wanaamini ni kuwaunganisha mama na mwana  kwa mara nyingine.
Bobbi Kristina, 21, amekuwa katika hali ya kutokujitambua tangu tarehe 31 Jan alipoookolewa akiwa amepoteza fahamu akiwa katika sinki la kuogelea nyumbani kwake.


0 comments:

Post a Comment